My Blog List
Wednesday, December 8, 2010
MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA UANDISHI WA FILAMU ZA KUTISHA.
Kuna uandishi wa aina nyingi wa miswaada ya filamu lakini linapokuja suala la uandishi wa filamu za kutisha na zile za kisayansi, waandishi wengi wanakumbana na changamoto mbalimbali na mwisho wa yote hushindwa kuwasilisha picha ya kile walichokusudia kuonyesha ama kusimulia.
Mambo yafuatayo ni ya msingi sana kuzingatia na hakuna budi kufuatwa hasa katika uandishi wa filamu za kutisha.
1. Andika katika Uasilia wake.
Kitu kinachotofautisha filamu nzuri ya kutisha na filamu mbaya ya kutisha ni uhalisia wake.filamu nzuri za kutisha ni zile zinazozingatia mawazo halisia na uwasilishwa katika uhalisia wake, na filamu mbaya za kutisha ni zile ujumbe wake ni ule wa kawaida na hauna mvuto kuanzia uwasilishaji wake na uhalisia wake kimandhari, kiasi kwamba mwandishi ahangaiki kuweka vionjo na ubunifu
Mwandishi yeyote wa filamu za kutisha anatakiwa kumbuka kuwa watazamaji wameshaangalia filamu nyingi za kutisha, na wasingependa kuendelea kuangalia filamu hizo hizo kwani ujumbe na uwasilishaji wake unachosha na hauna mvuto tena. Mwandishi bora wa filamu za kutisha lazima ahakikishe anaandika kitu chenye mvuto na ubunifu wake uwe ni wa hali ya juu ambao utamfanya mtazamaji akae kuanzia mwanzo mpaka mwisho wa filamu.
2. Kuwe na matukio mengi ya kutisha.
Mwandishi bora wa filamu za kutisha lazima matukio anayoyandika yamwogopeshe na yamtishe yeye kwanza, na daima ajaribu kupambana na matukio hayo ya kutisha, fanya hivyo ukiwa na lengo na madhumuni, kwani kwa kufanya hivyo ni dhahili kwamba matukio yote katika filamu uliyo iandika yatakuwa ni ya kuvutia. Zingatia; matukio yote yanayokutisha, yape uzito wa kutosha huku ukiongezea na ubunifu ili kuyapa uhai na uhalisia zaidi.
3. Andika kitu ambacho unafikiri hakijawahi kuonekana kwenye
Filamu.
Mwandishi wa filamu za kutisha anauwezo wa kuiandika filamu ambayo itafanikiwa au kufeli. Filamu zote bora za kutisha zinakuwa na tukio moja ambalo halijawahi kuonekana katika filamu yoyote ya kutisha.
Ni dhahiri kwamba sisi sote ambao tumeangalia/ tumekuwa tukiangalia filamu za kutisha kuna tukio moja ambalo tunalikumbuka na hatuwezi kulisahau hata kama tuliliangalia tungali watoto wadogo. Mwandishi wa filamu za kutisha anatakiwa kandika japo matukio matatu ambayo anafikiri ni mapya kabisa yenye uhalisia na ambayo hayajawahi kuonekana kwenye filamu yoyote ile, hiyo itafanya matukio hayo kudumu na kukumbukwa na watazamaji kwa muda mrefu na hivyo kuifanya filamu yako iwe ya kipekee.
4. Matukio katika filamu yawe na uhalisia wake.
Filamu nyingi za kutisha huwa hazibebi uasilia wake, watazamaji wanaangalia tu kwa sababu wanataka kitu cha kuangalia, ni jambo lisilofichika kwamba matukio mengi katika filamu hizi yanaonekana ni ya kutengenezwa na hayana ubunifu wowote ndani yake, hivyo kukosa mvuto kwa watazamaji, mwandishi wa filamu za kutisha anatakiwa kuandika kiasi kwamba wahusika, maneno na matukio yawe na uasilia wake katika maisha halisi ya jamii anayoiandikia.
5. Isiwe na mwisho wa kuchekesha
Changamoto kubwa wanayokabiliana nayo waandishi wa filamu za kutisha ni namna ya kuandika mswada wenye uasilia wake kuanzia mwanzo mpaka mwisho, waswahili wanasema “chumvi nyingi huaribu mchuzi” ni nadra sana kukuta watazamaji wakicheka hasa waangaliapo filamu nzuri ya kutisha bali kwa filamu mbaya ni rahisi, hakikisaha mswada unaoandika hautakuwa wa kuchekesha bali wenye ujumbe ulioshiba.
6. Angalia filamu nyingi za kutisha kabla ya kuanza kuandika ya kwako.
Si maanishi kwamba ukopi na kupesti au kuchukua kila kitu ulichokiangalia kwenye filamu, fanya hivyo kwa nia ya kujifunza na kuuweka sawa ubongo wako. Mwandishi bora wa filamu za kutisha ni yule anayeangalia filamu nyingi za kutisha kadri awezavyo, unashauriwa kuangalia filamu moja kila siku, la kuzingatia hapa ni uzuri na ubora wa filamu unazoangalia. Fanya hivyo kabla ya kuanza kuandika filamu ya kwako
7. Zingatia ugawaji na mpangilio wa matukio katika wa filamu yako.
Filamu nzuri ni ile inayoanza na matukio ya kuvutia, ni ukweli usiopingika kwamba dakika 10 za kwanza katika filamu ni ngumu sana kwa waandishi wa filamu za aina zote, ni katika dakika hizo kumi mwandishi anakazi ya kumshawishi mtazamaji asizime runinga yake na aendelee kuangalia filamu mpaka mwisho. Filamu bora ni ile iliyopangiliwa vizuri huku ikiwa na uwiano sahihi wa matukio ya kuvutia na yenye ubunifu kuanzia mwanzo mpaka mwisho wa filamu.
Kufanikiwa kwa mwandishi katika aina hii ya filamu, kunahitaji utafiti wa kina na wa hali ya juu, umakini katika kupanga matukio, ubunifu unaozingatia fani na maudhui.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment